Jumanne 6 Mei 2025 - 12:52
Tunaihesabu Uingereza kama mshirika mkuu wa Israel/ Simamisheni uuzaji wa silaha kwa Israel!

Israel tangia tarehe 2 Machi imefunga njia zote za kuingilia Ukanda wa Ghaza, na licha ya ripoti nyingi kuhusiana na njaa kali inayosababishwa na kivuli cha vita, Israel bado imezuia kuingia kwa aina yeyote ya misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taasisi moja ya misaada ya kibinadamu nchini Uingereza imetoa tamko kupitia mtandao wa kijamii X, ikitaka mauaji yanayoendelea Ghaza yakomeshwe haraka iwezekanavyo. Taasisi hiyo iliandika: "Biashara zote pamoja na aina yoyote ya uuzaji wa silaha kwa Israel lazima usitishwe mara moja, na Israel mhalifu lazima iadhibiwe bila kuchelewa."

Israel tangia tarehe 2 Machi imefunga njia zote za Ukanda wa Ghaza, na licha ya kuwepo kwa ripoti nyingi kuhusiana na njaa kali inayowakumba watu chini ya kivuli cha vita, bado imekuwa ikizuia kuingia kwa misaada yoyote.

Msemaji wa taasisi hiyo aliongeza kwa kusema: "Miezi miwili bila chakula, bila maji, bila mafuta! Hivyo basi, ubinadamu uko wapi? Madai ya wahisani wa kibinadamu yako wapi? Bado tunaiona serikali ya Uingereza kuwa mshirika mkubwa wa utawala huu wa kiuaji. Serikali ya Uingereza haipaswi kamwe kushirikiana na mnyama huyu katili."

"Badala ya chakula, nguo, au mahema ya malazi kwa ajili ya watoto na watu wa Ghaza, wao wanaendelea kuongeza mashambulizi ya anga."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha